TFF wajibu hoja za Michael Wambura
Shirikisho la soka nchini TFF limejibu tuhuma zilizotolewa na makamu wa rais wa shirikisho hilo Michael Richard Wambura, baada ya hukumu ya kufungiwa maisha kutangazwa dhidi yake na kamati ya maadili inayoongozwa na mwenyekiti Hamidu Mbwezeleni mapema hii leo.
Wambura alizungumza na waandishi wa habari kupinga hukumu iliyotolewa dhidi yake, huku akiweka wazi baadhi ya mambo ambayo anaamini yamekua mzizi wa yeye kufanyia figisu hadi kuingizwa hatiani.
Mdau huyo wa soka alidai kuwa, kuna mambo mengi yanaendelea ndani ya TFF likiwepo suala la ubadhilifu wa fedha, ambao umekua kinyume na utaratibu, jambo ambalo aliahidi kulitafutia siku la kulianika hadharani kupitia vyombo vya habari.
Jioni ya leo TFF imejibu tuhuma hizo kwa kutoa ufafanuzi wa kina katika kila kipengele ambacho kilizungumzwa na Wambura alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
No comments