Tukio hilo limethibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Yusuph Ilembo na kusema miili hiyo imeonekana leo majira ya asubuhi baada ya maji ya mto huo wa msimu kupungua.
Aidha, Kamanda Ilembo amewataja marehemu hao kuwa ni Ormins Sunguyo na mkewe Nembris Sunguyo ambao walikuwa na mtoto mdogo aliyefahamika kwa jina la Oloosukuta Sunguyo ambaye alinusurika kifo.
Kamanda Ilembo alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi katika mkoa wa Arusha kuchukua tahadhari kipindi hiki cha mvua na kuepuka kuvuka mito wakati maji yanafurika.