Header Ads

  • Breaking News

    Serikali yalivalia njuga tatizo la nguvu za kiume.


    Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo, jamii, jinsia na Watoto, Dk Faustine Ndugulile amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Afya akishirikiana na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), kufanya utafiti wa afya ya uzazi kwa wanaume ili kubaini sababu za tatizo hilo na kujua ongezeko la upungufu wa nguvu za kiume ni kubwa kiasi gani nchini.
    Ndugulile amefikia uamuzi huo kwani mara zote Serikali imekuwa ikitilia mkazo afya ya uzazi kwa mwanamke na kusahau upande wa pili.
    Amesema kwa upande wa Tanzania mpaka sasa hakuna tafiti zozote zilizofanyika juu ya tatizo hilo kwa wanaume, hivyo ni wakati wake sasa kulifanyia uchunguzi wa kina na kubaini suluhusho lake.
    Aidha kwa tafiti zilizofanywa kisayansi duniani zimebaininsha kuwa wanaume wengi wana matatizo ya nguvu za kiume sababu kubwa ikiwa ni mtindo wa maisha, kwani wengi wao hupendelea kula vyakula ambavyo si bora vyenye mafuta na sukari kwa wingi ambavyo kwa kiasi kikubwa huchangia magonjwa yasiyoambukizwa na ukosefu wa nguvu za kiume.

    No comments

    Post Top Ad

    Post Bottom Ad